BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Wednesday, August 31, 2011

EID NJEMA WADAU...

Napenda kuwatakia sherehe njema ya Eid El ftri wadau wote wa blog hii… wito wangu tuu serebrate kwa usalama na kuzingatia hasa yale yaliyoelezwa na Kova… No disco kwa watoto
Sikukuu njema…

Sunday, August 28, 2011

MAMTEI AMEJIPANGA VIZURI MWAKA HUU...



MSANII nguli wa Filamu nchini Cesilia Sengerema (Mamtei), ametamba kuwa mwaka 2011ni mwaka wake na anatarajia kufanya vizuri zaidi kwa kuwa amejipanga kikamilifu.
Hata hivyo Mamtei anasema sanaa kwake ni kazi kwa kuwa anaitegemea kwa asilimi 90 katika maisha yake.
Mamtei ambaye amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kushiriki tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, iliyoandaliwa na Chuzi entertainment, anasema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kujipanga vizuri ili aweze kumudu mazingira ya kazi zake.


Mamtei alijizolea sifa lukuki na kujikusanyia mashabiki wengi kutokana na umahiri wake katika kuigiza, jambo lililowafanya wapenzi wengi wa filamu kuvutiwa sana na vipande alivokuwa akiigiza.
“Kuonekana katika runinga bila mpango haina maana yoyote, ndio maana niliamua kuwa kimya ili nijipange, nahakikisha 2011 nitafanya kitu cha tofauti,”anasema.
Alisema ili kuonyesha ukimya wake kuwa uliku na jambo tayari Filamu yake ya Golden night ambayo ni zawadi ya mwaka mpya imeanza kusambazwa na kampuni ya steps entertainment.
Filamu hiyo ambayo kwa mujibu wa Mamtei alisema itakuwa tofauti na filamu nyingine zilizoingia sokoni hivi karibuni, kwa kuwa imewashirikisha wasanii wakongwe kama Monalisa na Natasha.
Monalisa ambaye ametamba katika filamu nyingi na pia aliyetunukiwa tuzo ya msanii bora wa kike katika tamasha la filamu Zanzibar (ZIFF) lililofanyika mwaka jana. Atashirikiana na mama yake ambaye naye pia ni mkongwe wa filamu (Natasha)
Alifafanua kuwa muunganiko huo ndio utakaoifanya filamu hiyo kuwa tishio kwani hakuna asiyejua kazi inayofanywa na wasanii hao wakongwe, ambao wamejizolea sifa ya kushirikishwa katika filamu nyingi na wasanii wenzao.


Aidha aliongeza kuwa, ili kuwapa raha wapenzi wake ambao hawajamwona kwenye uwanja wa filamu kwa kipindi kirefu, Aprili 2011 ataanza kurekodi filamu yake mpya ambayo alisema bado hajaipatia jina. 

Sunday, August 21, 2011

BEKA; kuja na tamthiliya


MSANII nyota wa bongo movies Bakari Makuka (Beka), amesema ataanza kucheza tamthilia ili kuibua vipaji vya wasanii wengi wenye maadili na kuwa nyakati hizi wasanii wakongwe wametosa mchezo huo.


Beka ambaye anaelekeza hisia zake katika kuiteka tasnia hiyo alijizolea sifa lukiki miaka ya 2002 alipokuwa katika kundi la Nyota Academia lililokuwa linaongozwa na msanii nguli wa filamu Singo Mtambalike (Richie).


Anasema, tamthilia zilizokuwa zinachezwa na wasanii kipindi hicho ziliweza kuwapatia wasanii mafunzo na maadili mazuri lakini sasa wasanii hao wanawatumia watu ambao hawana maadili katika kazi hiyo kwa lengo la kuuza kazi na sio kuipatia jamii ujumbe husika.


“Binafsi nimeanza kuzalisha filamu zangu lakini nitajikita zaidi kwenye tamthilia kwa sababu kwa sasa zimeachwa sana na ndio maana maadili ya sanaa hayafuatwi,” anasema.


Beka anaongeza kuwa, “Tulipokuwa kwenye vikundi vya maigizo (tamthilia) tulikuwa tunafundishwa maadili ya kazi na wasanii walioko kwenye gemu sasa hivi na waliopitia vikundi wanatambua, tatizo ni moja tu wasanii wakubwa hawawatumii watu wenye taaluma wanatoa kazi kwa mto ilimradi auuze tu,”.


Alisema, tamthilia zinazotakiwa kuchezwa zinatakiwa kubeba uhusika wa jambo na muwakilishi anapaswa kuuvaa uhalisia ili jamii iweze kupata ujumbe uliotarajiwa.


Beka anasema, tamthilia za aina hiyo zitafanikisha katika kuendana na ushindani wa soko la sanaa na kuwa wasanii kama Bi Kikokwa, Bi Mkora na wengine waliotikisa enzi hizo ni mfano wa kuigwa.


Anasema, katika kuwapata wasanii watakaocheza tamthilia hizo atatumia mfumo wa kupiga kura kwa kila jina litakalopendekezwa ili kazi iweze kufanikiwa zaidi.


“Nataka kuwa tofauti na wasanii wengine sitafurahia pale kazi yangu itakapopokelewa tofauti na jamii, cha msingi nitatumia mfumo wa kupiga kura kwa kila mtu ambaye atapendekezwa sio kuhonga lengo langu ni kurudisha hadhi ya tasnia ya filamu katika mstari wake,” anasema.


Aidha, Beka anasema tayari ameaanza kucheza filamu zake mwenyewe mbili na kuwa moja inaitwa I hate my wife ambayo imetengenezwa na kampuni ya Msekwa Media.

Saturday, August 20, 2011

SHAMSA APANIA KUMFIKIA OPRAH..


SHAMSA Ford ni msanii wa filamu nchini anayeingia kwa kasi katika tasnia hiyo huku akiwa na malengo ya kufikia mafanikio ya muongozaji maarufu wa vipindi mbalimbali vya televisheni nchini Marekani, Oprah Winfrey.


Shamsa ambaye jina la baba yake linafanana pia na jina la baba wa muigizaji maarufu nchini Marekani, Harrison Ford, ameanza kucheza filamu mwaka 2010 na kuweza kukubalika na watu wengi hasa waongozaji wa filamu ndani na nje ya nchi.



Anasema anatamani kuwa mwanamke wa heshima sana katika ulimwengu huu na baadaye kuwa muigizaji wa kimataifa kama ilivyo kwa Oprah winfrey muongozaji maarufu wa vipindi mbalimbali vya televisheni nchini Marekani.


“Maishani mwangu natamani vitu viwili tu, kuwa mwanamke wa heshima sana katika ulimwengu na muigizaji wa kimataifa. Tukizungumzia Oprah ni mwanamke anayeheshimika sana anauwezo wakufika hapa nchini na kuingia Ikulu kuzungumza na Rais na mawazo yake yakasikilizwa na kutekelezwa leo hii sisi wasanii wa Tanzania hatujaweza kufikia hatua hiyo natamani kuwa wa kwanza,” anasema.



Shamsa anasema, katika kipindi cha muda mfupi ambacho ameanza kuonekana kwenye filamu, ameona mafanikio na kwamba tayari ameanza kupata tenda za kucheza filamu nje ya nchi.

Sunday, August 14, 2011

TSJ YAANDAA MASHINDANO YA MISS & MR KWA MWAKA HUU....

SERIKALI ya wanafunzi ya Time School of Journalism (TISJOSO) kwa kushirikiana na kampuni ya kizalendo ya Zealot Entertainment Agency imeandaa mashindano ya urembo ya kumtafuta mshindi na mwakilishi ya kinyang’anyiro cha Miss na Mr TSJ 2011.
Shindano hilo litafanyika katika sherehe ya Welcome First Year Special Bash ambayo imelenga kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo kwa ngazi zote kuanzia Basic Certificate, Advanced Certificate na Diploma kwa mwaka huu.
Hafla hiyo ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza ambayo itapendezeshwa na mashindano haya inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 3 Septemba mwaka huu katika maeneo ya Jangwani Sea Breeze Mbezi beach.