BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

Promo

Promo

Wednesday, June 29, 2011

Grand Malt Open Film Festival


Meneja wa kinywaji cha Grand Malt bidhaa ya TBL Bi. Consolata Adam akiongea katika uzinduzi rasmi wa Tamasha la wazi la filamu Tanzania (Grand Malt Open Film Festival) katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga. Bi Consolata Adam amesema kwamba Wiki ya maonyesho ya wazi ya Filamu inaendelea mpaka tarehe 3 Julai Mwaka huu. Maonyesho hayo ya Filamu yanafanyika kwa mara ya tatu katika historia yake.

Meya wa jiji la Tanga Mzamil Shemdoe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la wazi la filamu Tanzania (Grand Malt Open Film Festival) katika viwanja vya Tangamano mjini Tanga Kulia ni Musa Kissoky mkurugenzi wa Sofia Production waratibu wa tamasha hilo na Kushoto ni Consolata Adam Meneja wa kinywaji cha Grand Malt bidhaa ya TBL ambao ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya filamu Tanzania.

Monday, June 27, 2011

SHOW OFF...

Let us luk for different celebrity poze today and find out who's gonna Rock all of them....

 haya fight a pose
una mrimember huyu??
 Yemesi
 Vanessa-Nzediegwu
 Ramsey Noah.
Mzee Kipara
pole Bambo...
 Kingwedu bado yupo??
 Ze komedi ileeee ya kipindi kileeee...

Saturday, June 25, 2011

DEVIL KINGDOM...


Cast:Steven Kanumba and Ramsey Noah
Director: Steven Kanumba
Writer: Ally Yakuti
Rating: PG-18
Running Time: 120 min.
Available in: VCD, DVD, VHS.
Produced in: 2011.
Synopsis:


A young man working hard to have it all in life but isn't very successful, looks at his peers which are multimillionaires and doesn't stop asking himself why he isn't as successful as they are. He begins questioning GOD, and wondering if is he not praying as much as the others and as a result he is not as rich!
He starts a church but it doesn't generate much income, and so he asks one of his millionaire friends how he can be successful like them. His friend opens up and tells him it’s not the work of GOD but that of another power. He tells him that if he wants to be like them he has to join their secret society. He agrees and they give him everything; healing power, an increase in the number of church members, money and the good life but in return he has to make some sacrifices! After some time he is required to sacrifice an albino, which he finds impossible, so the secret society tells him to sacrifice his parents instead, he then tries to quit but they tell him there is no getting out - once you're in, you're. So he goes back to his church and kneels before GOD.

FADHIL MAOGOLA AKIWA KAZINI

Ni mmoja katika ya wapiga picha bora hapa tz. moja ya kazi zake hapo down.....
Fadhili akishoot mojawapo ya movie ailizoshoot

Fadhili Maogola

testin'

Friday, June 24, 2011

AFRICA MAGIC SWAHILI KUANZA TRH 1 JULY.

Hivi karibuni kampuni ya kurusha matangazo ya Televishen kwa Digital ya DSTV  kupitia M-Net Africa wamezindua channel itakayojulikana kwa jina la Africa Magic Swahili, Channel hiyo itaanza kuwa hewani tarehe 1 July katika channel 127 katika decorder ya DSTV.

Na channel hiyo itaonyesha filamu za kiswahili,Comedy,Vipindi vya majadiliano vya kiswahili na miziki ya kiswahili.Akiongea na Wageni waliohudhuria hafla hiyo Mkurugenzi wa M-Net Africa Biola Alabi amesema yote ni kukuza lugha ya kiswahili na Filamu za kiswahili na michezo yote inayohusisha lugha ya kiswahili.

FILAMU YA GLAMOUR (The Reality Behind Dreams) KURUKA ZIFF 26 JUNE 2011.


KAMPUNI mahiri katika masuala ya utengenezaji filamu kwa hapa nchini ya ZG Films Usiku wa tarehe 26 mwezi huu wa sita 2011 kuanzi muda wa saa moja na robo , filamu yake ya Glamour: (The Reality Behind Dreams) itaonyeshwa katika tamasha hili la filamu la ZIFF na kuzinduliwa rasmi na kushuhudiwa na wageni mbalimbali wanaudhuria tamasha hili wakiwa wametoka nchi mbalimbali kutoka sehemu kubwa ya Ulimwengu huu.

ZG Films – Nyumba inayozalisha bidhaa bora za filamu Zanzibar ikiongozwa na mpiga picha mashuhuri na mtengenezaji wa filamu, Javed Jafferji – tayari ameshazindua taarifa kadhaa zinazohusiana na masuala muhimu na matukio ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania. Hivi karibuni amezindua Journey to the State House: The Life of Seif Shariff Hamad ikiwa na maana ya Safari ya Ikulu: Maisha ya Seif Shariff Hamad, ambayo itakuwa toleo la mwanzo katika Tamasha la ZIFF 2011(Zanzibar International Film Festival) ambayo imeingia kwa ajili ya tuzo ya filamu bora katika tamasha hilo.

ZG Films ikiwa na lengo la kuangalia athari na ufikaji wa sekta ya filamu Tanzania, ina lengo la kuwafikishia watu kimataifa, kwa kuweka kiwango cha kimataifa katika sekta hiyo hapa Tanzania. Katika kutimiza lengo hili, ZG Films and Media House, wakishirikiana na Zanzibar International Film Festival, inatoa, filamu ya Glamour (The Reality Behind Dreams)
Filamu hii imetayarishwa na Javed Jafferji na kuongozwa na Amitabh Aurora, Glamour: The Reality Behind Dreams ni filamu ya kwanza ya ZG Films and Media House, ni filamu ya Bongo ya Kisasa ikihamasishwa na Swahili Fashion Week – Tukio kubwa Tanzania linalohusiana na uwanamitindo, na kutoa ukweli juu ya sekta ya uwanamitindo, Mhusika mkuu katika filamu hii sio mwengine bali ni Eva Issac (aka “Eva ya Diva”), mmoja kati ya wanamitindo wakubwa Tanzania.

UJIO MPYA...

Yvonne Nelson
Miezi ya nyuma, mwigizaji  wa kike kutoka nchini ghanaYvonne Nelson alipigwa marufuku kwa mwaka mmoja kuonekana ama kuigiza katika filamu kutokana na tabia aliyofanya ambayo ilikuwa ni unprofessional katika certain movie.
Yvonne Nelson
Katika maandalizi yake kurudi tena amejiandaa vilivyo na kwa sasa ameonesha moto wake kwa kuachia baadhi ya promo photos kwa mashabiki wake hebu nawe jitazamie kama mdau.

 Yvonne Nelson

INI EDO NA EGO OKOYE WAPIGANA LOCATION

Ini Edo na Oge Okoye.
Imeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Nigeria kuwa mastaa wa kike maarufu nchini humo wameshambuliana wakiwa location maeneo ya Festac Town, Lagos.

Ini Edo
Kulingana na chanzo cha habari, ugomvi huo ulianza baada ya kudaiwa INI mshitaki rafiki yake wa zamani Oge kuwa alikuwa akimpiga jicho la kimahaba mume wake, inasemekana kwamba Oge hakuyapokea vizuri malalamiko hayo yaliyo pelekea kuzuka kwa ugumvi mkubwa ambayo ulisababisha ku cancel shughuli nzima ya kushoot iliyokuwa inaendelea huko festac Town, Lagos.
Oge Okoye.
Ripoti kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari inaonyesha kwamba Edo INI na Oge Okoye  wameshiriki katika ugomvi wakiwa location Festac Town, Lagos.

Wednesday, June 22, 2011

SPORAH ASAINI MKATABA MPYA NA LIME HOUSE STUDIO.


Mtangazaji  wa kipindi cha The Sporah Show Sporah Njau amekamilisha kusaini mkataba na studio ya Lime House kufanya kazi pamoja katika kipindi chake.
Sporah Njau
Akielezea hisia zake kupitia mtandao wa kijamii wa facebook Sporah alisema. Nanukuu
·         “AT LAST I OFFICIALLY SIGNED MY CONTRACT WITH LIME HOUSE STUDIO..! GREAT NEWS.. I ABSOLUTELY LOVE WORKING IN THE STUDIO & WATCHING MAGIC HAPPEN!... BUT..!!
BY SIGNING MY CONTRACT, I WILL NOT ALLOW TO HAVE ANY OTHER BRAND APART FRM "SPORAH"
BECAUSE I HATE SAYING .."IT JUST ISN'T MEANT TO BE" I WILL NOT STOP.
WE WILL TERMINATE OUR NEW BABY "iMAGAZINE" TO "THE SPORAH MAGAZINE"
THANK YOU ALL FOR YOUR SUPPORT.” Asema Sporah.
Sporah Njau

Mkataba hu aliosaini na Lime House utambana kufanya kazi na kampuni ama kipindi kingine zaid ya kipindi chake hicho cha “THE SPORAH SHOW”


Sporah Njau

Tuesday, June 21, 2011

Mercy Johson na Hubby wake Kufanya shopping yanguo za harusi New York.

Mercy nchini USA
Imekuwa kawaida kwa wadada hawa wa tasnia yua filamu nchini Nigeria kuwa pamoja kwa kile kinachosemekana uhusiano wa jinsia moja..
Mercy
Sasa hii kali msanii Mercy Johnson inasemekana yuko Nchini Marekani akifanya shopping ya mavazi ya harusi ya nne na huyo mdada walie nae katika mahusiano..
Mercy akichagua nguo
Chekshia walivyojiachia..
mercy na hubby wake.

Monday, June 20, 2011

GENEVIEVE NNAJI akiwa GHANA azungumzia kuhusiana na muvi mpya ya JAMES BOND.

Genevieve Nnaji
Taarifa za chini chini zinaeleza kuwa Msanii nyota wa filamu nchini Nigeria Genevieve Nnaji anatarajia kucheza filamu na Msanii maarufu na Nyota kutoka USA James Bond.
James Bond

Genevieve aliwahi kuonekana na Robert De Niro ambaye ni Actor,Director na Producer kwenye Cannes Film Festival na kuzungumza mambo mengi na imeelezwa kuwa huenda akaungana na actress kama Teri Hatcher,Halle Berry na Jane Seymour.
Genevieve Nnaji
Hivi Karibuni Genevieve Nnaji  alipata mwaliko weekend hii kwenda Accra  nchini Ghana katika uzinduzi wa filamu kutoka kwa Director Obi Emelonye iitwayo “The Mirror Boy”

Katika Ziara yake hiyo alitembelea vituo mbali mbali vya habari na kufanya Interview mbalimbali na nyingi zilihoji kuhusiana na taarifa zilizopo kuwa yeye kucheza katika filamu mpya ya James bond.
Wengi walimuhoji kuwa inamgharimu sana na kumweka attention kuigiza muvi hiyo.

Kitu alichowambia waandishi na watangazaji ni kuwa Yuko makini na anazingatia Script atakayopangiwa na si actor mwenzake anayeigiza nae.
Na alikazia kwa kuzungumzia tena kauli yake ya ki philosofia ambayo kila mara husema "you can only delay destiny but you can’t stop"

Genevieve Nnaji alizaliwa May 3, 1979 Mbaise, Imo state nchini Nigeria na akakulia Lagos. Akiwa kama muigizaji wa kike aliwahi kushinda tuzo mwaka 2005 ya African Movie Academy Award kama Mcheza filamu bora wa Kike amabaye kito cha CNN kilimfananisha kama Julia Roberts wa Afrika. Akiwa na Miaka kumi na Tisa aliingia rasmi katika tasnia ya filamu na muvi ya “Most wanted”

Sunday, June 19, 2011

Filamu nyingi za Bongo zinakosa uhalisia

Kanumba akiwa na Aunt ezekiel
Filamu nyingi za Kibongo zimekuwa zikikosa mvuto hasa kwa watu makini wanaozitazama kutokana na waigizaji wengi kusahau majukumu yao ya uigizaji na badala yake kutafuta ufahali kwenye filamu zao.
Kuna maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kama vile kwa nini wasanii wetu wanapenda kutumia majumba ya kifahari, moja je ni ushamba au ulimbukeni, pili je ni hali ya umaskini ambao unatokana na famila nyingi za Watanzania?
Sababu za kufikiria hayo zimetokana na ukweli kwamba Watanzania wengi tumetokea katika nyumba za kawaida hivyo wasanii hao wanakuwa na fikra mgando wakifikiria iwapo wataigiza katika nyumba za kawaida filamu hazitavutia.
hemed
Wapo wengine wanaokuwa wanafikiria kwamba wakitumia nyumba za kawaida hawatauza na kuonekana tofauti na wengine.
Kuna wale wenye fikra mgando wakitumia fursa hiyo ya majumba ya kifahari wakiamini hawana uwezo wa kuyamiliki.
Wapo ambao walioathiliwa na hali ya umaskini ambao wamejikuta wakiathirika kisaikolojia wakifikiria kuonekana kwenye majumba ya kifahari ndipo watauza zaidi na konekana wa thamani machoni mwa mashabiki wao.
Wasanii wa hapa nchini wanajikuta wakitumia magari ya kifahari yenye bei za kutupwa kama vile Hammer, Vorg na mengine ya aina hiyo.
Wasanii hawa wamekuwa wakienda mbali huku wakisahau hata filamu zao zinakuwa na maudhui ya namna gani.
Waigizaji wetu wameshaathiliwa na kuigiza maisha ya kitajiri wa kupitiliza hali iliyowafanya wakati mwingine hata watazamaji kujikuta kushindwa kutazama filamu na kubaki kuangalia magari na majumba wanayotumia.
Tatizo kama hilo limeikumba tasnia hii kwa wale wanaokuwa waigiza kama mabosi hata kama ofisi ya kawaida lakini wamekuwa wakionekana wamepigilia suti kila wakati.
Yusuph mlela
Kwa mfano utamkuta mwigizaji anaigiza kama Afisa uhusiano wa benki ya NBC kila muda anapoonekana iwe nyumbani njiani amevalia suti ya gharama.
Hali kama hiyo inafikia nasema kuwa huu ni ushamba watu kama hawa ndiyo wanauwa wabishi hata kuigiza filamu zinazoonyesha mazingira ya vijijini au kuwa mfanyakazi wa ndani.
Huu usharobaro umesababisha hata wakati wanapokuwa wanapiga picha za mwigizaji akiwa anaamka usingizini akiwa amejipigilia urembo usoni ‘make up’.
Ushauri wangu tuu ni kwamba ili tuweze kuingia kikamilifu katika soko la filamu kimataifa ni lazima tuweze kuweka uhalisia kwanza ndipo tuanze kuonesha matumizi ya hivyo vitu vya thamani.
Wasanii wanatakiwa watambue kuwa watazamaji wao wanatoka maeneo mbalimbali na wengi ni wale wenye uwezo wa hali ya chini na kawaida ambao hawana uwezo wa kumiliki magari au majumba ya aina hiyo hali ambayo inawasababishia kushindwa kuangalia filamu na kubaki kuangalia aina ya gari, umba au suti aliyovaa msanii.
Ester Flavian
Wasanii wanatakiwa wawe makini kutazama aina ya hadithi wanayokuwa wanaigiza na si kutazama aina ya vitu wanavyotumia vina thamani ya aina gani na kujikuta mwisho wa siku wakishindwa kujikita katika hadithi husika.
Esterflavian,Daud michael,'Ramsey wa bongo,na Raulant Anthon 

Majina ya Kiingereza Filamu za Kibongo ni Ushamba?


NI jambo la kufurahisha sana kuona kuwa hivi sasa tumekuwa tukijitahidi kujitutumua na kupiga hatua katika uandaaji wa filamu hapa nchini.
Si tu kuwa inafurahisha bali pia inatia moyo na kuleta fahari kwetu Watanzania kwani katika kipindi cha miongo mingi, tumeonekana kuwa nyuma katika fani mbalimbali za sanaa.
Chimbuko lililopo sasa la utitiri wa filamu hizi na zile za Kizalendo, linadhihirisha mbio za dhahiri shahiri zenye dhati ya kuelekea kilele cha mafanikio ya kweli katika soko la filamu.
Lakini licha ya mbio hizo, kuna jambo moja ambalo kwakweli ni kero kwa mashabiki na wapenzi wa filamu hizo za Kibongo kwa ujumla ambazo zimezalishwa na waandaaji, wasambazaji pamoja na wazawa ambao ni Watanzania wenyewe.
Nalo si jingine bali ni hii desturi ya filamu nyingi, kama si zote zinazofyatuliwa sasa kuwa na majina ya Kiingereza huku yanayoonekana ndani yameigizwa katika mazingira pamoja na lugha ya Kiswahili.
Binafsi nimekuwa nikijiuliza mara nyingi tatizo ni nini? Ni ulimbukeni wa Lugha, kudharau lugha yetu ya Kiswahili inayokua kwa kasi au nini?
Labda pengine mnaiga kutoka katika mataifa Fulani, lakini kama ndivyo, mtakuwa mnakosea sana, kwa sababu kila taifa lina mila, desturi na utamaduni wake katika masuala mbalimbali, hasa ya burudani ambayo ni sehemu ya kielelezo cha taifa.
Kutokana na hali hiyo, hata wanunuzi wa nje wanaponunua na kukuta kilichoandikwa nje si kilichomo ndani, wengi wamekuwa wakitushusha Watanzania wote.
Hivyo kwa ushauri wa bure kwa wasanii wetu, wawe makini na majina ya Kiingereza wanayoyanadi katika makasha yaende sambamba na hadithi husika, vinginevyo tutabaki kuwa malimbukeni wa lugha za watu.
Mbona hapo awali katika michezo ya kuigiza, tamthilia pamoja na filamu za waliowatangulia hakukuwahi kutokea kitu kama hicho wa kuidhihaki lugha yetu na walisikika na kuvutia, hata sasa tunawakosa sana.
Kwa kuthibitisha hilo, hata sasa tunashuhudia wasanii wakongwe wengine waliosalia kama vile Said Ngamba ‘Mzee Small’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ wanavyoendelea kukienzi Kiswahili chetu ambapo katika filamu na tamthilia zao zote mwendo ni wa kizalendo pekee.
Nawauliza wasanii wetu wa kizazi kipya kwanini msiige kutoka kwao? Au ndiyo mnaendekeza ile dhana ya kuwa wamepitwa na wakati na wenye mawazo yaliyokwishakuwa ya kizamani! Fahamuni kuwa mnapotea kwa kuelekea mahali ambako siko tunakokuhitaji.
Nikiwa mdau wa burudani, nachukua fursa hii kuviomba vyama pamoja na mabaraza yanayohusika na usimamiaji wa masuala ya filamu, kulitazama hili kwa macho makini ili kuepuka athari kubwa inayoweza kutokea hapo baadaye.
Pia nawaomba wahusika wenyewe ambao ni watayarishaji pamoja na waigizaji kuhakikisha wanakienzi Kiswahili chetu kwa kuachana na ulimbukeni wa kutoa filamu zenye majina ya Kiingereza.


Saturday, June 18, 2011

'MAOGOLA' MIAKA 12 KATIKA SHUGHULI YA KU-SHOOT VIDEOS Kinachomkela ni dharau kutoka kwa wasanii.

Camera man fadhili maogola.
Fadhili Maogola ni mmoja wa baadhi ya watu wanaojihusisha na shughuli za uchukuaji wa picha za Video na za mnato (Cameraman). Alijiingiza rasmi katika tasnia hii mwaka 1999 chini ya kampuni ya Cool Multmedia na baadae alihamia katika kampuni ya Kijitonyama Upendo group (KUG) akiwa kama camera man na Editor  wa video. Akiwa hapo alifanya kazi nyingi  kama kurekodi video za nyimbo za injili zikiwemo album mbalimbali kama “ Mungu Anakupenda”, “ Bam Bam”  kutoka Kijitonyama Upendo Group Choir,  “Uwe macho” ya rose Muhando, “Mapito ya Bahati Bukuku na nyingine nyingi, ambapo anaeleza baada ya kukomaa katika kazi hii alianzisha kampuni yake binafsi.

Focus media company ni kampuni yake binafsi aliyoianzisha na kuisajili serikalini mwanzoni mwa mwaka huu 2011. Chini ya kampuni yaake amefanya documentary na filamu mbalimbali zikiwemo Question mark, Adhabu ya kaburu ambazo zintarajiwa kutoka hivi karibuni. Mbali na filamu hizo pia amefanya Documentary mbalimbali na watu tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchio. Pia akiwa kama mpiga picha wa kujitegemea amewahi kufanya kazi na Hemed katioka filamu ya “Johnson”, amefanya na Yusuph Mlela katika filamu ya “Mtumwa wa mapenzi” na pia amefanya kazi na wasanii wengine wengi kama Jackline Wolper, Mzee Magali, Miriam Migomba na pia amefanya na daudi Michael katika filamu ya “More than Crazy”.

Fadhili Maogola ambaye ni motto wa sita katika familia ya mzee Maogola, alizaliwa miaka 33 iliyopita na kupata elimu yake hapahapa Dar es Salaam na kufikia kidato cha nne baada ya hapo alijiunga na kozi ya electronics katika chuo cha VETA, fadhili ameeleza kuwa kwa sasa bado anasema katika chuo kimoja nchini Kenya Nairobi kinachotoa elimu ya video Production. Kwa upande wa maisha yake binafsi Fadhili ana mchumba na alibahatika kupata watoto mapacha wa kike na wakiume ambao ni Faiza fadhili na Fahami fadhili.

Akizungumzia kuhusiana na Changamoto mbalimbali wanazopata camera Man, alisema kuwa anakerwa sana na dharau kutoka kwa wasanii, anasema kuwa CameraMan anaonekana ni mtu wa mwisho hivyo hata mapato wanayopata ni kidogo nah ii inasababishwa sana na wengi wao kutokuwa na elimu ya ufanisi wa fani hiyo( sio professional). Hivyo alishauri kwa wapiga piccha wenzake wajifunze, na watafute ushauri kwa waliotangulia katika kazi hii na pia wafahamu mambo yanayowahusu katika Production kwani Cameraman sio kujua kushika na  kuwasha camera tuu bali kuna vitu vingi, alisema fadhili.

Katika mazungumzo Fadhili Maogola alizungumzia kuhusiana na mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu na kusema “ Napenda kuongelea mmmomonyoko wa maadili katika ngazi tatu yaani kwa waandishi wa habari, vyombo vyo habari na wasanii uchwara. Zamani katika Radio na television nyimbo zisizo na maadili zilikuwa  hazichezwi lakini sa hivi wadau hawazingatii maadili hayo wanaonesha mambo yasiyofaa. Kwa waandishi wanaharibu jamii kwa kuandika habari chafu mfano uchangudoa na hata wanatoa picha chafu katika magazeti. Wasanii nao sa hivi wamepoteza maadili maadili wanaona furaha kupiga picha za uchi na kuzitoa katika baadhi ya magazeti ninaomba kushauri hawa wote wajirekebishe” alisema Fadhili.
Fadhili alipenda kuwashukuru baadhi ya wadau walimsaidia hata kimawazo hadi hapo alipofika kuweza kumiliki kampuni yake binafsi Focus media Company, watu hawa ni kama Mzee Kidai, fanuel Ndonde, Christian Kika, marehemu Mzee Hamir Rajab, Rose Mhando na meneja wake Nathani Wami kwa mchango wao anawashukuru. Aliwashauri wasanii watambue umaarufu utakuja tuu na si kwa kukaa uchi na aliwasili wanaopenda kuwasiliana nae hata kuomba ushauri na kikazi zaidi watumie 0712 515145 ili kukuza tasnia nzima ya sanaa na muziki kwa ujumla.

FILAMU MPYA YA MORE THAN CRAZY SOKONI MWEZI HUU.

Msanii wa filamu Daudi Michael.
Msanii wa filamu hapa nchini Tanzania, Daudi Michael amekamilisha utengenezaji wa filamu yake itakayo tambulika kwa jina la “More than Crazy”. Daudi Michael amesema kuwa yuko katika hatua za mwisho za kufanya mazungumzo na baadhi ya wasambazaji na mambo yakienda vizuri anatarajia kuingiza sokoni filamu hiyo mwezi huu wa sita. Filamu hii ya “ More than Crazy”  inazungumzia dhuruma kwa ndugu wa damu na pia kwa upande mwingine inahusu usaliti katika mapenzi kutokana na ugumu wa maisha. Daudi Michael amesema kuwa filamu hii ni ya saba kutengeneza chini ya kampuni yake ya D Production, ambayo ndani ya filamu  hii amecheza na baadhi ya nyota wa filamu kama vile Ester, Mzee Magari, Baambucha na Sudi Ally.

Msanii huyu Daudi Michael alijiingiza rasmi katika sanaa ya maigio mwaka 2007 mwezi  wa 9 siku ya Ijumaa, chini ya kundi la maigizo la Bahari Arts Group, kundi ambalo hujihusisha na kutengeneza filamu na tamthiliya mbalimbali. Kundi hili lilikuwa likisimamiwa na mwalimu Adam Joseph pamoja na Japhari Makatu amabao Daudi Michael anaeleza hawa  watu ndio chachu ya mafanikio yake hadi sasa kwani walimpatia elimu ya sanaa vya kutosha.
Daudi Michael akiwa na Msanii Heliety Kahembe.

Akizungumzia kuhusiana na Tasnia ya filamu na sanaa ya maigizo kwa ujumla Daudi Michael anasema kuwa “Sanaa ni maisha ya mwanadamu yeyote aliyeko duniani, naamini kila Mtanzania anaweza kuwa msanii kwa sababu hayo tunayocheza ni maisha halisi ya watanzania na napenda tuu kuwashauri wasanii wasikurupuke na watambue kuwa ni muhimu sana kupata elimu ya sanaa” Daudi alieleza.

Nilipofanya mazungumzo naye nilimuhoji kuhusiana na hali iliyo katika sanaa kwa nini wasanii wengi hasa maproducer hutumia majina ya kiingereza katika filamu zao kwa mfano filamu zake. Daudi allisema kuwa yeye aliangalia uelewa, upokeaji wa watu na kuhusiana na filamu zilizoandikwa majina  ya kiingereza na kugundua kuwa ‘majina ya Kiswahili hayana  mvuto, pili yanajaza eneo katika uandishi na pia lugha ya kiingereza ni lugha ya kimataifa na wanunuzi na wasambazaji ambao ni wahindi hupenda kununua filamu wanazozielewa majina. Na kitu cha mwisho ni kwamba walianzisha tasnmia nzima ya filamu walianza na lugha hii” alisema daudi.
Daudi Michael akiwa na Esther Flavian.
Alipozungumzia kuhusiana na nini wadau wa filamu watarajie kutoka kwake na neon lake la mwisho kwa wadau Daudi alisema kuwa anamtanguliza Mungu katika kila hatua anayofanya na alisema kuwa kampuni yake imejipanga vizuri crew nzima na aliwasihi wadau watarajie kazi nzuri kutoka D Production ambayo ndiyo kampuni yake anayoimiliki. Pia aliwasihi wadau wa filamu wapende kufanya research wasikurupuke na aliwaomba watanzania wa wadau wote kwa ujumla wapokee kazi zake na pia palipo na makosa washiriki kwa kumpa maoni kwa kuwa katika kila filamu zake hutoa namba za simu ili aweze kupata ushauri mbalimbali.

D Production ni kampuni yak wake mwenyewe daudi Michael na ina Crew ya watu mbalimbali akiwemo Kenny Aichi ambaye ni Editor, faridu Nankape na Fadhili Maogola ambao ni Camera man, Santana ni production Manager, Bora Arphani ni make up manager. Pia alisema chinio ya D Production alishatoa zaidi ya filamu sita ikiwemo Season of love, Noway out alizotoa mwaka huu na zingine nyingi tangu alipoanzisha kampuni hii rasmi mwaka 2008 alipotoa filamu ya Upside Down.